WEKEZA MARATHONS

Schedule

Sun, 20 Sep, 2026 at 01:00 pm

UTC+03:00
Location

Kisutu, Dar es Salaam | Dar Es Salaam, DS

Advertisement
WEKEZA MARATHONS | WEKEZA MARATHONS
WEKEZA MARATHONS ni harakati ya kijamii, kielimu na kiafya inayolenga kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kuthamini afya njema na kuwekeza kama njia endelevu ya kupambana na umaskini, kukuza ustawi wa kifedha, na kujenga mustakabali salama wa maisha.
Kupitia mbio za marathon, WEKEZA MARATHONS hutumia michezo kama chombo cha kuamsha fikra, kuelimisha, na kuunganisha jamii katika safari ya mabadiliko ya kiuchumi.
WEKEZA MARATHONS imejengwa juu ya dhana kwamba umasikini hauondoki wenyewe, bali kwa kuukimbia kwa kufanya mabadiliko ya tabia, kuwekeza katika maarifa sahihi, na kufanya uwekezaji wa kifedha wa muda mrefu.
Mafanikio ya kifedha yanahitaji nidhamu, uvumilivu, maandalizi, na uamuzi wa kuanza safari bila kusubiri mazingira yawe kamili.
Dhana Kuu (Concept)
WEKEZA MARATHONS inatokana na falsafa kwamba uwekezaji ni safari ndefu hivyo mbio za marathon zinawakilisha safari ya maisha ya kifedha ambapo mshiriki hujifunza nidhamu,uvumilivu,kakabili changamoto, na kuendelea mbele hata pale anapochoka ili lengo lake litimie.
Kwa kutumia mbio kama lugha rahisi, WEKEZA MARATHONS huwasilisha elimu ya uwekezaji kwa namna inayoeleweka kwa wananchi wa kawaida, bila istilahi ngumu za kifedha, na kwa kuzingatia uhalisia wa maisha ya Watanzania.
Malengo ya WEKEZA MARATHONS:
Malengo makuu ya wekeza marathons ni kujenga utamaduni wa uwekezaji miongoni mwa Watanzania kwa kuunganisha afya ya mwili, elimu ya fedha, na mshikamano wa jamii katika mapambano dhidi ya umaskini.
Pamoja na hayo imedhamiria;
Kuelimisha jamii kuhusu misingi ya uwekezaji kwa lugha rahisi na mifano halisi.
Kuhamasisha wananchi kuanza kuwekeza hata kwa mtaji mdogo.
Kukuza uelewa wa tofauti kati ya akiba na uwekezaji.
Kujenga nidhamu ya kifedha na mtazamo wa muda mrefu.
Kuwezesha wananchi kuunganishwa na taasisi halali za uwekezaji.
Kukuza afya ya mwili na akili kama nguzo ya mafanikio ya kifedha.
Kuibua kizazi kinachotambua uwekezaji kama sehemu ya maisha ya kila siku.
MAANA YA KAULIMBIU YETU;
Kimbia Umasikini, Kimbilia Uwekezaji
(Run from Poverty. Run to Investment.)
“Kimbia Umasikini, Kimbilia Uwekezaji” ni wito wa mabadiliko ya fikra na vitendo.
Ni kauli mbiu inayohamasisha:
kukataa umaskini wa fikra na mazoea,
kuchukua hatua za makusudi kuelekea uwekezaji,
na kuanza safari ya kujenga uhuru wa kifedha.
Kauli mbiu hii inaunganisha moja kwa moja harakati za kimwili (kukimbia) na harakati za kiuchumi (kuwekeza), na kuifanya WEKEZA MARATHONS kuwa zaidi ya tukio na kuwa movement.
Kaa tayari kwa jambo hili adhimu.
Tarehe 20 mwezi wa 9 mwaka 2026,
Rasmi WEKEZA MARATHONS itafanyika.
Kutakua na Mbio za 5KM, 10KM na 21KM
Mafunzo mafupi ya elimu ya uwekezaji.
Ushauri wa kifedha wa moja kwa moja
Ushirikiano na taasisi mbalimbali za uwekezaji
Bila kusahau kupata connections na burudani.
Wekeza marathons imeratibiwa na Meza ya uwekezaji
Tunawakaribisha wadhamini na washiriki katika kufanikisha tukio hili 💥💥💥
Mkurugenzi
Naytham S Masoud
0746465095
Advertisement

Where is it happening?

Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania

Event Location & Nearby Stays:

Know what’s Happening Next — before everyone else does.
Meza ya uwekezaji
Host or PublisherMeza ya uwekezaji

Ask AI if this event suits you